© Radio Kwizera, Ngara-Tanzania
search this site the web
search engine by freefind

Back to Home

RADIO KWIZERA

Wednesday 02- Jun-2010

BIHARAMULO

Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani kagera inatarajia kuitumia zaidi ya shilingi milioni 290 kwa ajili ya kutengeneza barabara za wilaya hiyo zenye urefu wa kilomita 120

 

Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Bw Mahona Sambo amesema shilingi milioni 53 kati ya hizo zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara za mjini

 

Amesema fedha zilizobaki zitafanya matengenezo ya barabara na makalvati katika maeneo ya vijijini

 

Bw sambo amesema kazi hizo ambazo zitafanyika mwaka huu zitatahusu matengenezo ya kawaida, maeneo korofi pamoja na ujenzi wa Makalvati

 

NGARA

Mganga wa hospitali ya Nyamiyaga wilayani Ngara, Bw. Misago Senyamanza, ametangaza nia ya kugombea nafasi ya udiwani wa kata ya Mugoma, wilayani humo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

 

Bw. Misago, ambaye ametangaza kugombea kupitia chama cha mapinduzi CCM amesema ameamua kuwania nafasi hiyo ili kushirikiana na wakazi wa  kata ya Mugoma kuharakisha  maendeleo yao.

 

Amesema maendeleo ya kata hiyo yamebaki nyuma kwa muda mrefu hivyo ameahidi kuwa endapo atachaguliwa atashirikiana na wakazi wa kata hiyo kuharakisha maendeleo

 

Bw. Misago, aanakuwa mwana CCM wa pili kutangaza nia ya kugombea udiwnai wa kata ya Mugoma baada ya Diwani wa sasa Bw George Rubagora kutangaza pia nia  ya kutaka kuendelea na wadhifa huo.

 

KASULU

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF linatarajia kuanza kutoa mafunzo ya stadi za maisha kwa watoto wanaoishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mtabila iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

 

Mkuu wa makazi wilayani Kasulu Bw Fredrick Nsajile amesema hayo katika kikao cha kutambulisha mpango huo wa UNCEF ulioanzishwa baada ya kubaini kuwa watoto wa kambi hiyo wanaishi katika mazingira hatarishi

 

Amesema kambi hiyo iliyofungwa rasmi june 30 mwaka jana haina shule hivyo watoto kukosa cha kufanya na wengine kwenda kufanya kazi katika maeneo mbalimbali

 

Bw Nsajile amesema UNICEF imechukua jukumu hilo ili kuwasaidia watoto wanaojiingiza katika vitendo viovu kama vile kuvuta bangi na wizi kutokana na kukosekana kwa mfumo rasmi wa elimu

 

Kambi ya mtabila iliyofungwa mwaka jana ina jumla ya wakimbizi elfu 36 na kati yao watoto ni aslimia 50

 

NGARA.

Mkazi wa Kijiji cha Kanazi Wilayani Ngara Gilbert Nyamblomba  amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kupatikanana hatia ya kujaribu kuiba Pikipiki

 

Akisoma hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ngara, Bw Geofrey Biyereza amesema mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.

 

Awali mwendesha Mashitaka wa polisi Bw. John Kessy amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo March 11 katika kijiji cha Kanazi wilayani Ngara

 

Amesema mshitakiwa alitaka kunyang’anya pikipiki aina ya Sanlag yenye namba za usajili T. 495 BCM mali ya Bw. Oswad Nyamlomba ambaye ni ndugu yake

 

MULEBA

Wanachama wawili wa CCM, Prof Anna Tibaijuka na bw Alfred Tibaigana wametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Muleba Kusini linaloongozwa na Bw Wilson Masilingi.


Bw Tibaigana ambaye alikuwa Kamanda Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, amekabidhi barua yake kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Wilbroad Musafiri, muda mfupi baada ya Prof Tibaijuka kutangaza nia

 

Bw Tibaigana amekanusha uvumi ulioeneka kw awananchi kwmaba amejiondoa katika kinyang’anyiro hicho

 

Amesema kuna kundi linalosambaza uvumi kuwa amebadili nia, huku akidai kuwa baadhi yao wanawapotosha wananchi kuwa atakwenda kugombea jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam.

ARUSHA

Waziri Mkuu, Bw Mizengo Pinda, amesema ni muhimu kwa wananchi wa Afrika Mashariki kuelezwa maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili waweze kunufaika nayo.

 

Bw Pinda amesema hayo jana wakati alipotembelea kuona ujenzi wa makao makuu ya ofisi za Jumuiya hiyo unaondelea mjini Arusha.

 

Amesema wananchi ambao ndio wenye Jumuiya waelezwe kila hatua na wafahamu mwelekeo wa jumuiya  ili waweze kunufaika

 

Aidha waziri mkuu amesema kuanza kwa ujenzi huo kunaonyesha dhamira ya viongozi wa nchi tano wa Jumuiya hiyo kwa kujenga umoja kati yao wenye nguvu na kuwaletea maendeleo wananchi wao.

KIGALI

Wakili wa Mwanasiasa wa Rwanda Bi Viktwar Ingabire amepelekwa hospitali baada ya kulalamika kuwa na matatizo ya moyo

 

Wakili huyo Peter Elinder ambaye anashikiliwa kwa tuhuma za kukanusha kuwepo kwa mauaji ya halaiki, alipelekwa katika hospitali ya Mfalme Faisal mjini Kigali ambako uchunguzi ulionyesha kwamba hana tatizo la moyo kama alivyodai

 

Maofisa wa polisi wa Rwanda wamesema, Wakili huyo raia wa marekani anaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kukanusha kuwepo kwa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994


Bw Elinder aliingia nchini Rwanda wiki moja iliyopita ili kumwakilisha Bi Ingabire ambaye pia anakabiliwa na mashitaka ya kukanusha kuwepo kwa mauaji ya halaiki pamoja na kushirikiana na makundi ya magaidi

 

29th May 2010

BIHARAMULO

Mkazi wa kata ya Runazi wilayani Biharamulo mkoani kagera amaefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo akikabiliwa na tuhuma ya kumtorosha mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Mlimani

 

Mbele ya hakimu Gabriel Mariki Mwendesha mashitaka wa polisi  bwa Boniface Mayala amemtaja mshitakiwa kuwa ni Hamis Ramadhani  

 

Amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo May 15 mwaka huu katika eneo la Kijiji cha Ng’ambo wilayani Biharamulo ambako alimchukua msichaan huyo na kumepeleka katika kata ya Runazi

 

Amesema mshitakiwa alimtorisha msichana huyo kwa lengo la kufanyia kazi za ndani

 

Mshitakiwa amekana shitaka lake na kupelekwa rumande ambapo kesi yake itatajwa tena June tisa  mwaka huu.   

...........................................................................................

NGARA

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Ngara wameipongeza  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa uamuzi wake wa kuwahoji wanasiasa wanatoa pikipiki, baiskeli na zawadi nyingine  katika majimbo.


wakazi hao wamesema hayo kufuatia maelezo yaliyotolewa jana Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah  kuwa taasisi yake ina orodha ya waliogawa pikipiki, baiskeli na zawadi nyingine

 

Wakiongea na radio kwizera kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema baadhi ya watu waliotangaza nia ya kugombea ubunge wilayani humo wamekuwa wakitoa vitu mbalimbali kinyume cha sheria

 

Wakazi hao wamesema hatua hiyo ya TAKUKURU inapaswa kuchukuliwa haraka ili kudhibiti vitendo hivyo na kuwa zawadi hizo hutolewa kwa nia mbaya kwani hulenga makundi fulani ya watu

.................................................................................................................................................

BIHARAMULO
Watoto watatu wa familia moja katika kijiji cha Katerela, Kata ya Biharamulo mjini mkoani Kagera wameteketea kwa moto walipokuwa wamelala usiku wa kuamkia juzi


Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Bw Henry Salewi, amesema tukio hilo limetokea wakati watoto hao wakiwa wamelala kwenye nyumba peke yao, kwani wazazi wao walikuwa wamelala nyumba ya  jirani.


Kamanda Salewi amesema, jitihada za kuwaokoa watoto hao zilishindikana kutokana na moto kuwaka kwa kasi katika nyumba hiyo

 

Pia amesema uchunguzi wa awali wa tukio hilo unaonyesha watoto hao walilala usingizi na kuacha moto walioukoka wenyewe ukiendelea kuwaka kwenye jiko la mafiga na baadaye kushika kwenye nyasi za nyumba hiyo.
.................................................................................................................................................
 

MISUNGWI

Mamia ya watu wakiwa na silaha za jadi wamevamia na kuvunja kituo cha kidogo cha polisi cha kata ya Mbarika, wilayani Misungwi mkoani mwanza na  kuwaua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi.

 

Tukio hilo limetokea juzi saa 1:30 jioni wakati raia hao wakiwa na silaha kama vile mapanga, rungu na mawe walipovamia kituo hicho.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Siro, askari polisi wawili wa kituo hicho, walizidiwa nguvu na wananchi hao, hali iliyosababisha kukimbia ili kuokoa maisha yao.

 

Amesema Majambazi hayo yalikamatwa wakati yakijiandaa kufanya uhalifu na kufikishwa kituoni hapo lakini baadaye wananchi walivamia kituoni na kuwaua watu hao

.................................................................................................................................................

DAR ES SALAAM

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imelikataa ombi la viongozi wa dini kutaka uchaguzi mkuu ujao usifanyike siku ya Jumapili kama ilivyopangwa na tume hiyo.

 

Mkurungezi wa Uchaguzi, Bw Rajabu Kiravu, iamesema uamuzi huo umezingatia utamaduni wa  muda mrefu wa kupiga kura siku ya Jumapili.

 

Amesema tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961, chaguzi zote zimekuwa zikifanyika siku ya Jumapili, isipokuwa mwaka 2005 ambapo tume hiyo, ililazimika kuahilisha kutokana na kifo cha mmoja wa wagombea

 

Amesema kwa kawaida vituo vya kupiga kura hufunguliwa kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na kuwa mpiga kura anaweza kuweka utaratibu wa muda ambao ataona unamwezesha kusali na kupiga kura

.................................................................................................................................................

KINSHASA

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limepiga kura ya kuidhinisha kuondolewa kwa walinzi wake  elfu mbili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC ifikapo June 30 mwaka huu

 

Hata hivyo baraza hilo limeahirisha uamuzi wa kuwaondoa askari wake elfu 20,500 kama ilivyopendekezwa na Rais Joseph kabila wa DRC

 

Uamuzi wa kuwaondoa asakari wote wa umoja wa mataifa kutoka DRC utatolewa mwaka ujao kwa kuzingatia hali ya usalama ilivyo nchini humo

 

Kadhalika baraza hilo limeongeza muda wa vikosi vya ke nchini DRC hadi June 30 mwaka kesho

.................................................................................................................................................

KIGALI

Jeshi la Polisi nchini Rwanda Jana limemkamata wakili Peter Erlinder kutoka marekani kwa tuhuma za kukanusha kuwepo kwa mauaji ya halaiki

 

Wakili huyo amewasili nchini humo kwa ajili ya kumtetea mwanasiasa Bi Viktwar Ingabire anayeshitakiwa kwa ugaidi na kukanusha kuwepo kwa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 ambapo zaidi ya wtau laki tano waliuawa

 

Msemaji wa Jeshi la Polisi la Rwnada Bw Eric Kayiranga amesema wakili huyo amekamatwa jana asubuhi

 

Amesema wakili huyo kutoka Marekani anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa uchunguzi

...................................................................................................................................................................................

NEW YORK

Wanachama wa mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha za nyuklia wamekubaliana kuhakikisha kuwa eneo la mashariki ya kati halina silaha za nyuklia

 

Wanachama wa mkataba huo waliokutana mjini New York wametaka kuitishwa mkutano mwaka 2012 ambapo nchi za mashariki ya kati ikiwa ni pamoja Iran zitakutana kufikia azma hiyo

 

Aidha makubaliano hayo yameitaka Israel kujiunga katika mkataba wa kuzuia kusambaa kwa silaha za nyuklia

 

Rais Barack Obama wa Marekani ameunga mkono hatua hiyo lakini amepinga hatua ya kutengezwa kwa Israel kwani italipelekea taifa hilo kushbindwa kuhudhguria mazungumzo ya mwaka 2012

Kikwete Na Ardhi.

Rais Jakaya Kikwete, amewaagiza wananchi wanaoishi kandokando ya barabara za lami nchini kutokubali kurubunika kuuza mashamba yao kwa wageni kwa lengo la kuwekeza.

Rais Kikwete ametoa  agizo hilo jana wakati wa  uzinduzi wa barabara ya Horohoro Tanga   yenye urefu wa kilomita 65 itakayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi  bilioni 78.05.

,Rais Kikwete amesema kutokana na kuboreka kwa barabara nchini watu kutoka maeneo mbalimbali watafika katika eneo la kijiji cha Mikocheni  wilaya ya Tanga kwa nia ya kutaka kuwekeza.

Amesema  wananchi wanapaswa kuchangamkia fursa za kiuchumi za nchi za Afrika Mashariki zitakazotokana na kuimarika kwa barabara zilizo karibu na maeneo yao  ili waweze kujikwamua na umaskini .

Rais Kikwete ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kutoa kiasi cha dola milioni 698 kupitia taasisi ya Millenium (MCC) kwa kipindi cha miaka mitano katika shughuli za maendeleo nchini.

 

Barabara hiyo inajengwa na Kampuni ya Sinohydro Corparation Ltd kutoka nchini China ambayo  ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Aprili 2012.EndS

.......................................................................

 

KIBONDO

Uongozi  wa zahanati ya Rugunga kata ya  Kitahana  wilayani  Kibondo   umeiomba halmashauri ya wilaya  hiyo kujenga choo na tanuru la kuchomea   taka.

 

Mganga  mfawidhi wa  zahanati hiyo  Bw  William Kanyungu amesema    choo cha zahanati hiyo kilichojengwa  mwaka  1983  kinakaribia  kujaa

 

Naye mhudumu wa afya  katika zahanati hiyo  Bi  Liberatha Nchana amesema  wanahitaji tanuru la  kuchoma  takataka  zinazopatikana katika zahanati yao

 

Aidha  Bi   Nchana   amesema    takataka  zote zinatakiwa zichomwe  moto hivyo halmashauri  haina budi  kushughulikia tatizo hilo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza                                                  

NGARA.

Mkazi wa Kijiji cha Kanazi Wilayani Ngara Gilbert Nyamblomba  amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kupatikanana hatia ya kujaribu kuiba Pikipiki

 

Akisoma hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ngara, Bw Geofrey Biyereza amesema mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.

 

Awali mwendesha Mashitaka wa polisi Bw. John Kessy amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo March 11 katika kijiji cha Kanazi wilayani Ngara

 

Amesema mshitakiwa alitaka kunyang’anya pikipiki aina ya Sanlag yenye namba za usajili T. 495 BCM mali ya Bw. Oswad Nyamlomba ambaye ni ndugu yake

 

 

KIBONDO

Serikali wilayani Kibondo imewataka  wakazi wa wilaya hiyo kupanda miti  na kuacha  tabia  ya kilimo cha kuhama hama ili kudhibiti uharibifu wa mazingira

 

Mkuu wa wilaya ya Kibondo Bw Dan Makanga  amesema hayo jana wakati akizindua maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo wilayani Kibondo imefanyika katika kijiji cha Biturana

 

Katika hotuba iliyosmwa kwa niaba yake na Katibu tawala wa wilaya ya Kibondo Bw Julius Samwely, mkuu huyo wa wilaya amesema  jamii iepuke tabia za kukata miti ovyo, kuchoma moto na kulima katika vyanzo  vya maji

 

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya mazingira ni “Tunza mazingira ya asili kwa hifadhi endelevu ya viumbe hai”    EndS

MULEBA

Wanachama wawili wa CCM, Prof Anna Tibaijuka na bw Alfred Tibaigana wametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Muleba Kusini linaloongozwa na Bw Wilson Masilingi.


Bw Tibaigana ambaye alikuwa Kamanda  Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, amekabidhi barua yake kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Wilbroad Musafiri, muda mfupi baada ya Prof Tibaijuka kutangaza nia

 

Bw Tibaigana amekanusha uvumi ulioeneka kw awananchi kwmaba amejiondoa katika  kinyang’anyiro hicho

 

Amesema kuna  kundi linalosambaza uvumi kuwa amebadili nia, huku akidai kuwa baadhi yao wanawapotosha wananchi kuwa atakwenda kugombea jimbo la Kawe jijini  Dar es Salaam.

 

BUNDA.

 

Mkazi wa Kibara wilayani Bunda mkoani Mara amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba kutokana na kinachosadikiwa kuw ani ugomvi wa kimapenzi

 

Kamanda wa polisi mkoani Mara Bw Robert Boazi amesema tukio hilo limetokea May 31  katika wilaya ya Musoma vijijini ambako mtu huyo alikwenda kwao na mke wake aliyetambuliwa kuwa ni  Esther Daniel.

 

Kamanda Boazi amemtaja aliyejinyonga kuwa ni Paul Ngawia mwenye umri wa miaka 30 ambaye kabla ya atukio hilo alikuwa ametengana na mke wake na alikuwa amekwenda kumtaka mkewe arejee nyumbani.

 

Amesema hakuna mtu aliyekematwa kuhusu tukio hilo na kwmaba polisi wanaendelea kufanya uchunguzi                              

 

 

DODOMA

Kanisa la Anglikana Tanzania (ACT) limesema litawanyang’anya mavazi ya kiaskofu ambayo yamekuwa yakitumiwa vibaya na watu wanaojiita maaskofu wa Kanisa jipya la Kiinjili la Anglikana Tanzania.
 

Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Mwita Akiri, ametoa taarifa hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu habari kuwa kanisa hilo limemeguka


Dr Akiri amesema wataandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Msajili wa Vyama vya Hiari ili wasisajili kanisa hilo mpaka litakapofuta jina la Anglikana, kwani liko kinyume cha taratibu za usajili.

Amesema Serikali itasaidia kuwapa uelewa wananchi kuhusu ujio wa Kanisa hilo lenye lengo la kuleta uvunjifu wa amani kwa Kanisa Anglikana  Ends


 

KIGALI

Zaidi ya raia elfu 17 wa Rwanda wanaoishi nje ya nchi hiyo wamejiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa rais wa taifa hilo uliopangwa kufanyika mwezi Augist mwaka huu

 

Katibu mtendaji wa Tume ya uchaguzi ya Rwanda Bw Charles Munyaneza amesema jana kuwa idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka

 

Amesema idadi hiiyo imeongezeka kutoka elfu 16 waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa rais wa Mwaka 2003

 

Bw Munyaneza amesema tume ya uchaguzi ya Rwanda itaendelea kuwahamaisha raia wake walioko ndani na nje ya nchi ili kushiriki uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Agiost tisa mwaka huu